Jiandae Kuishi Peke Yako Baada Ya Maisha Ya Chuo

Jiandae Kuishi Peke Yako Baada Ya Maisha Ya Chuo

Na MICHAEL ANDERSON

Kabla na baada ya masomo ni muda wa kuwaza maisha ya baadaye (Life after you graduate)

After spending upwards of three years away, the idea of moving back home can seem ideal to some, but to others, less so.

Maamuzi haya graduates wengi huwa hawazingatii sana lakini amini nakwambia huwa wengi wanafanya hili kosa bila kujua na hugharimu miaka kadhaa ya bila faida dhidi ya elimu zao

You won't be glad to know that most of the deals can't be supportive to your career staying there while struggling so far away looking for a condusive place to stay. Look for a place now!

Kuna mafanikio ambayo yanahitaji milango ya pesa, kuna yanayohitaji milango ya mawazo, kuna yanayohitaji milango ya connection na yanayohitaji eneo.

Kuna watu wanawaza nitaenda kwa mjomba nikauze dukani, wengine kwa shangazi nimsaidie kusimamia miradi yake, wengine kwa wazazi wangu wao wanitafutie kazi au wanipe mtaji n.k.

Usijilaumu wala hakuna anayekulaumu, lakini kujua tulikotoka ni vizuri ili itusaidie kujifunza tunakoelekea.

FIKIRIA HAYA,

Kama upo dilemma until now where to go jaribu kuanza kufikira pia unganisha na hizi zitakusaidia sana katika kuanza baada ya miaka mitatu ya chuoni

  1. Account yako ya bank ya chuo usiipuuze, ile uliokuwa unawekewa boom, ebu iendeleze itunze, pindi ukimaliza chuo hakikisha haiishiwi pesa isije kufungiwa.

Anza kuplan biashara ndogo ndogo halali, biashara ndogo ndogo haihitaji experience acha uoga na kuona aibu utakosa hata sabuni. Ukipata faida toa kidogo peleka kwenye account huwa ina heal akili.

  1. Epuka kutembea masafa marefu (safari) bila jambo la mhimu, mfano utoke Mbeya kwenda kusalimia ndugu Arusha kisa una pesa ya nauli , kumbuka unaweza kupata mchongo wa maana ukakosa nauli.

 

 

 

  1. Kujitolea ni muhimu sana kuliko jambo lolote wakati huo, sio mbaya kama location inaruhusu ukaishi na kujitolea huku ukifanya kitu cha kukupatia nauli daily. Kwenye kujitolea sio lazima ujitolee specifically kwenye career yako, angalia hata kitu kinacho relate.

 

  1. Set na update CV yako iwe up to date all the time,ni mhimu sana. Ifanye simu yako kama mtoa taarifa za ajira kwa kutumia ajira apps na jitahidi kusoma matangazo ya ajira ili upate uzoefu. Hata kama sio career yako tuma maombi kila unapoona una fit au una relate kuna faida sana.

 

  1. Hakikisha mahusiano yako yana amani hasa kwa mabinti na vijana pia ukiona mchumba wako haeleweki ndiyo huwa wakati wenyewe huu usishangae, uki base kwenye mapenzi kipindi hiki utaumia sana.

Kwa kuwa hiki ndiyo kipindi cha kuachana na marafiki wa chuo na kila mtu kwenda zake, lakini utaona wengi wakifanikiwa na mlikuwa nao, jitahidi uvumilie maisha ni mipango anza sasa na wewe kujipanga.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags