Alichopitia Ommy Dimpoz Na Tekno Alipitia

Alichopitia Ommy Dimpoz Na Tekno Alipitia

Moja ya changamoto aliyowahi kupitia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo,'Ommy Dimpoz' ni tatizo la koo, lililomfanya apumzike kwenye muziki kwa muda. Hata hivyo inaelezwa kuwa naye msanii wa Nigeria Tekno alikumbwa na tatizo kama hilo.

Utakumbuka 2018, Ommy alifanyiwa upasuaji mkubwa wa koo Afrika Kusini baada ya kugundulika kuwa liliathiriwa na kinywaji.

Baada ya upasuaji wa kwanza kugonga mwamba msanii huyo alifanyiwa tena upasuaji wa pili mwaka 2019 nchini Ujerumani. Katika kipindi hicho, Dimpoz alishindwa kuimba kwa muda mrefu. Lakini baada ya miaka kadhaa alirudi tena katika fani yake ya muziki akitoa nyimbo kama "Ni Wewe", "Kata", na "Dede".



Hata hiyo mbali na mkali huyo mwaka 2018 naye mkali wa Afrobeat aliyekuwa akitamba na ngoma kama ‘Wash’, Duro, Diana na Pana, Tekno Miles naye alikumbana na tatizo la koo lililopelekea kusitisha kuimba kwa muda.

2018, Tekno aligunduliwa na tatizo linaloitwa Acid Reflux, ambapo alisafiri mpaka Marekani kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji ambao ulidaiwa kuwa mgumu kiasi kwamba baada ya operesheni hiyo, hakuweza kupumua vizuri.

Aidha baada ya kupona, Tekno alirejea kwenye muziki taratibu. Mwaka 2023, alifanya comeback kubwa kwa kushirikiana na Kizz Daniel kwenye wimbo wa "Buga", ambao ulikuwa hit Barani Afrika



Licha ya changamoto hiyo ya kiafya ambayo imepelekea msanii huyo kupoa kwenye gemu mazima. Lakini ameendelea kuwa mmoja wa waandishi na watayarishaji wakubwa wa muziki wa Afrobeats, akihusika na nyimbo kubwa za wasanii kama Davido, Drake, Beyoncé, Swae Lee na wengine wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags