Kanye West ametangaza kuirejesha ibada yake ya Jumapili inayofahamika kama Sunday Service ambayo itafanyika Machi 16, 2025.
Kupitia ukurasa wake wa instagram ameshea baadhi ya mazungumzo aliyofanya na mkurugenzi wa kwaya hiyo Jason White.
"Sunday Service inarudi machi 16, 2025" aliandika Ye kupitia instastory yake.
Ibada hiyo inarejea baada yakutofanyika kwa takribani miaka mitano baada ya kusimama januari 2020 kufutia mlipuko wa virisi vya Corana nchini Marekani
Hata hivyo, ibada hiyo ambayo ilifanyika kwa mara ya kwanza Januari 6, 2019 inarejea ikiwa ni kufuatia kejeli alizo toa rapa huyo dhidi ya Wayahudi mapema mwaka huu.
Sunday Service ni kundi injili la Marekani linalomilikiwa na rapa Kanye West 'Ye' huku likiongozwa na mkurugenzi wa kwaya hiyo Jason White. kundi hilo ambalo mwaka 2019 lilifanya ibada kila jumapili ndani ya dakika 60.
Rapa huyo na kwaya yake ya injili hutumbuiza nyimbo zake kubwa zaidi kila Jumapili wakati hafla hiyo inapofanyika, ambapo huimba mbele ya kundi la wasomi, familia na marafiki maarufu.

Leave a Reply