Kanye awapigia Diddy, Durk wakiwa Gerezani

Kanye awapigia Diddy, Durk wakiwa Gerezani

Rapa kutoka nchini Marekani, Kanye West 'Ye' amefanya mawasiliano kwa njia ya simu na nguli wa Hip Hop duniani Sean Diddy Comb 'Pdiddy' pamoja na rapa Lil Durk ambao wanashikiliwa Gerezani kwa makosa tofauti.

Kanye ambaye ameingia kwenye trend tena baada ya video yake akiongea na Lil Durk kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Wakati akizungumza na Durk, aligusia mipango ya album yake mpya 'Bully' inayotarajiwa kutoka, Juni, 2025. Kupia maongezi hayo alifichua kuwa dakika tano zilizo pita alizungumza na Diddy pia.

Lil Durk alikamatwa Oktaba, 2024 kwa tuhuma za mauaji ya kulipia kwa binamu wa rapa Quando Rondo mwaka 2022 na kwa upande wa Diddy alikamatwa Septemba 16, 2024 akikabiliwa na mashitaka ya unyanyasaji wa kingono.

Utakumbuka, miaka ya hivi karibuni Kanye amekua akifanya kampeni mbalimbali za kuwasaidia watu weusi waliopo jela, waachiwe huru na hivi Februari, 2025 alimuomba Rais wa Marekani Donald Tramp kumuachia Diddy.

Kupitia ukurasa wake wa X, Kanye aliandika "realDonaldTrump, tafadhali mwachilie ndugu yangu Puff."

Inaelezwa kuwa, kiasili Kanye na Durk hawakuwa sawa kwani Kanye alianzisha kampeni nyingi akuwaomba viongozi wa nchi ya Marekani wamuache huru Larry Hoover ambaye ndiye kiongozi wa Genge la 'Gangsta deciple' kambi kuu pinzani ya rapa Lil Durk. Lakini baada ya Durk kukaa karibu na Kanye akaanza kubadilika na kuanzisha kampeni mbalimbali katika mji wa Chicago za kumaliza vurugu za magenge zilizokuwa zikisababisha vifo vya watu wengi wasio na hatia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags