Tazama mwanamuziki wa Singeli, Baba Kash akiwarusha mashabiki katika viwanja vya Ngome Kongwe, Stone Town kisiwani Unguja.
Je kwa vibe hili la mashabiki kutoka mataifa mbalimbali linaenda kuthibitisha maneno ya wasanii wa Kenya Bien na Blinky Bill kuwa Singeli ndiyo muziki utaoleta Tuzo ya Grammy Bongo?
“Singeli ni muziki wa kipekee sana una 'sound' ambayo ni asili ya Tanzania. Mada ambazo zinaimbwa kwenye ngoma za singeli zingine ni vichekesho, zingine zinafundisha naiona tuu inaweza ikawa 'sound' ambayo inaweza trend World Wide. Singeli inaweza kuleta Grammy mbio sana ifanyie mixing, ifanyiwe mustering nzuri iandikwe vizuri katikati iwekwe tu mistari kidogo za kizungu kuwakilisha global,"alimesema Bien
"Mimi naujua muziki mzuri, sijawahi kuona mdundo mzuri kama wa Singeli. Muziki huo unaweza kuipatia Grammy Tanzania unachotakiwa ni kuwekeza na kuutengeneza kwa muundo ambao unaweza kupenya kimataifa," alisema Blinky Bill wakati akizungumza na Mwananchi
TAZAMA VIDEO HIYO KUPITIA INSTAGRAM YA @Mwananchiscoop

Leave a Reply