Maumivu Ya Tumbo Yamfanya Shakira Ahairishe Show

Maumivu Ya Tumbo Yamfanya Shakira Ahairishe Show

Mwanamuziki kutoka Colombia, Shakira ameahirisha moja ya show yake nchini Peru kutokana na tatizo la tumbo ambalo lilimfanya alazwe hospitali.

Nyota huyo anayetamba na ngoma ya ‘She Wolf’, mwenye umri wa miaka 48, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi kuwa alilazwa hospitalini wikiendi hii iliyokwisha jambo ambalo lilipekea kushindwa kufanya ziara yake ya ‘Las Mujeres Ya No Lloran’.

“Ninasikitika kuwajulisha nyote kwamba usiku wa jana ilibidi niende kwenye chumba cha dharura kutokana na tatizo la tumbo na kwa sasa ninalazwa hospitalini. Ninasikitika sana kutoweza kupanda jukwaani leo, wamenieleza kuwa siko katika hali nzuri ya kutosha kutumbuiza,” ameandika Shakira

Shakira alifuta tamasha lake la Jumapili, Februari 16, alilopanga kulifanyika katika Uwanja wa Taifa wa Peru ambalo lilikuwa la kwanza kati ya maonyesho mawili mfululizo katika mji kutokana na maumivu hayo makali huku akidia kuwa huwenda akaweza kutumbuiza leo Jumatatu, Februari 17 jijini Lima.

Las Mujeres Ya No Lloran ni jina la albamu mpya ya Shakira, ambayo inamaanisha "Wanawake Hawalii Tena" kwa Kiswahili. Lakini pia ni jina la ziara yake ya kimataifa iliyoanza Februari 11, 2025 huku ikitarajiwa kutamatika 30 Juni 2025 huko San Francisco, Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags