Jinsi Ya Kutengeneza Juisi Nzuri Ya Nanasi

Jinsi Ya Kutengeneza Juisi Nzuri Ya Nanasi

Mwili unapokosa kinga imara, unakuwa katika hatari ya kushambuliwa na kila aina ya magonjwa, lakini nanasi lina sifa ya kukabiliana na hali hiyo.

 

Nanasi ni moja kati ya matunda yenye vitamini, madini na virutubisho vingi vinavyoupa mwili nguvu na kuepuka kushambuliwa na maradhi.

 

Tunda hilo lina virutubisho vingi ikiwamo vitamin A, B na C na ina madini ya chuma, calcium na phosphorous na potasium, ambayo ni muhimu katika afya ya binadamu na mara kwa mara, linasaidia kuupa mwili kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali hasa pumu na shinikizo la damu.

 

Ili kuhakikisha kila mtu anapata virutubisho hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakilichukulia tunda hilo kama fursa ya kujipatia maokoto kwa kutengeneza sharbati.

Basi bila hiyana nami ndugu yenu nimekuja kuwaelekeza namna ya kutengeneza juisi hiyo nawewe uweze kupata maokoto.

 

Mahitaji

  1. Nanasi kubwa 1-3 (inategemea unataka kutengeneza juisi kwa kiasi gani siku hiyo)
  2. Tangawizi moja kubwa
  3. Sukari kiasi (hapa kwa wale ambao sio vipenzi wa sukari basi usiweke kabisa kwani tunda hilo lina asili ya sukari nyingi)
  4. Liamo moja kubwa (sio lazima kama unapenda juisi yako iwe na uchachu ndio utaweka maji ya limao)
  5. Maji lita moja
  6. Hiriki ya unga au vanilla (hapa ukikosa hivyo unaweza kutumia passion pia litakuletea ladha nzuri).

 

Namna ya kutengeneza

  1. Chukua nanasi lako lioshe vizuri na ulimenye vizuri, hakikisha haubakizi maganda yoyote.
  2. Baada ya hapo andaa bakuli lako kubwa kisha anza kukata vipande vidogo vidogo, halafu sagia tangawizi na passion kama utapenda kuweka, lakini pia utaweka na sukari yako ikikupendeza.
  3. Kisha utachanganya mchanganyiko wako na baada ya hapo utatia kwenye Brenda na uanze kubrendi mpaka pale itakaposagika vizuri.
  4. Ukishamaliza kubrendi juisi yako yote chukua chujio, chuja na uweke katika chombo kisafi, kisha utaiweka katika Friji ipate ubaridi.

Mpaka kufikia hapo juisi yako itakuwa tayari kwa ajili ya kunywa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags