Lakini hivi karibuni amezua mijadala katika mitandao ya kijamii baada ya kuamua kuziondoa kabisa nywele hizo. Hata hivyo kupitia video aliyoichapisha katika Instagram ameeleza sababu ya kufanya hivyo akitaja kuwa ni ujio wa filamu yake mpya.
“Sijawahi kunyoa ndevu kwa zaidi ya miaka sita, na sasa nimeamua kuziacha ziende. Ndevu hizi zimekuwa sehemu yangu kwenye filamu nyingi nilikuwa nazo nikiwa Khal Drogo kwenye Game of Thrones, pia nikiwa Aquaman.
Lakini leo nimeamua kuachana nazo. Sababu kubwa ni kwamba nataka mabadiliko, na pia kwa ajili ya kazi yangu kwenye filamu mpya, Dune 3, ambayo nafanya tena chini ya uongozi wa rafiki yangu Denis Villeneuve hii nimeifanya kwa ajili yake,”amesema
Aidha kutokana na hilo mashabiki mbalimbali wametoa maoni yao huku wakionesha kushitushwa na kitendo hicho wakiandika “Hizo ndevu ndizo zilikuwa zinafanya kazi kubwa sana,” “Rudisha ndevu tafadhali, bila hizo unakuwa tofauti,”
Huku wengine wakiandika “Unaonekana kijana kwa miaka 10 kuliko zamani,” “Umefanya jambo la maana, unaonekana freshi na ujumbe wako wa mazingira ni muhimu,”
Ingawa kunyoa kwake kulizua gumzo na mijadala katika mitandao ya kijamii lakini ukweli ni kwamba Momoa hakupoteza mashabiki wowote kama ambavyo baadhi ya watu wanavyorepoti.
Jason Momoa ni mmoja ya waigizaji mahiri ambapo amewahi kuonekana katika filamu mbalimbali ikiwemo Aquaman (2018), Justice League (2017), Conan the Barbarian (2011), Fast X (2023) na nyinginezo.
Leave a Reply