Tasnia ya filamu na burudani Korea Kusini imepata pigo baada ya taarifa za kifo cha mwigizaji maarufu Kim Sae-ron (24) aliyefariki dunia nyumbani kwake jijini Seoul.
Kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini humo, mwili wa msanii huyo uligunduliwa na rafiki yake jana Jumapili Februari 16, 2025 na kutoa taarifa Polisi.
Polisi wamesema kuwa uchunguzi wa awali haujaonyesha dalili za uhalifu, lakini wanaendelea kuchunguza mazingira ya kifo chake.
Kim alizaliwa Julai 31, 2000, na alianza safari yake ya sanaa akiwa na umri wa miaka tisa kupitia filamu A Brand New Life (2009), ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa.
Aidha aliendelea kung’ara zaidi kupitia filamu The Man from Nowhere (2010), ambayo ilimfanya kuwa miongoni mwa waigizaji chipukizi wenye mvuto mkubwa katika tasnia ya filamu ya Korea Kusini.
Katika miaka iliyofuata, alishiriki katika filamu zingine kubwa kama ‘A Girl at My Door’ (2014) na tamthilia za televisheni zikiwemo ‘Secret Healer na Leverage’.

Leave a Reply