Pastor Tony Kapola ahaidi kumsaidia Hashi Papi, Makonda atoa neno

Pastor Tony Kapola ahaidi kumsaidia Hashi Papi, Makonda atoa neno

Pastor Tony Kapola ahaidi kumsaidia matibabu, na kumtafutia nyumba mwanamuziki chipukizi wa Arusha aitwaye Hashi Papi.

Ahadi hizo zimetolewa baada ya kijana huyo kutumbuiza usiku wa kuamkia leo Desemba 29, 2024, mkoani Arusha katika tamasha la burudani ya vichekesho lililofanywa na Churchill Show kutoka nchini Kenya.

"Mimi ni kijana mdogo kama wewe RC amesema atafanyia kazi kwenye kile ambacho unakipenda, lakini kwa kuwa ni msanii nafikiri asifanye kazi nyingine na azingatie kwenye muziki. Lakini pia naahidi nitakutafutia nyumba utakaa na hayo meno ambayo ulipoteza tutakupeleka kwa wataalamu wa meno na watayarudisha," amesema Pasto Tony.

Hata hivyo kwa upande wake Makonda alisema ni vyema kuwashika mkono vijana wenye uhitaji kama Hashi Papi ili waweze kusonga mbele na kufikia ndoto zao.

"Kwangu mimi hiki ndio ninacho pigania zaidi, nafasi niliyopewa iwe na mchango kwa watu wengine na ndiyo maana nilimwambia Churchill kuwa Arusha tunawatu wenye vipaji lakini mazingira yanawakwamisha, naomba niwashauri watu wangu sio tu huyu mtaani kwako kama kuna mtu ana kipaji unajukumu la kumsapoti na siyo kumkatisha tamaa" amesema Paul Makonda

Mbali na hayo wachekeshaji wengine walioshiriki kwenye tamasha hilo ni Mathayo Saul, Tumbili, Mr Logic, Chipukeezy, Mzee Shayo, Tricky, Profesa hapo Erick Omond na wengineo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags