Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Anjella ameweka wazi kuwa kwa sasa anaacha kabisa kuimba nyimbo za Bongo Fleva huku akidai kuwa anarudi kumtumikoa Mungu.
“Bye Bye Bongo Fleva hatutaonana tena Narudi madhabahuni pa Mungu”ameandika Anjella
Kufuatia na kauli hiyo baadhi ya wadau na mashabiki wamemjia juu kupitia mitandao ya kijamii wakidai kuwa msanii huyo anatafuta kiki huku wengi wao wakimpongeza kwa hatua hiyo aliyoichukua.
Anjella alianza kupata umaarufu mwaka 2021 baada ya kusainiwa katika lebo ya Konde Music Worldwide, inayomilikiwa na msanii Harmonize.
Kwa upande wa Bongo Fleva Anjella amekuwa akitamba na ngoma zake kama Kioo, Kama, Nimekumisi, Blessing, Sina Bahati na nyinginezo.
Leave a Reply