Sasa Utaweza Kuweka Mitandao Ya Kijamii Kwenye Whatsapp Yako

Sasa Utaweza Kuweka Mitandao Ya Kijamii Kwenye Whatsapp Yako

Ikiwa ni mwendelezo wa maboresho katika mtandao wa WhatsApp ambao unadaiwa kuwa na watumiaji wengi zaidi, sasa wameweka program mpya ambayo itawasaidia watumiaji wake kuweka linki za mitandao yao ya kijamii kwenye profile zao za WhatsApp.

Awali program hiyo ilikuwa ikipatikana katika WhatsApp Business pamoja na WhatsApp GB huku kwa watumiaji wa WhatsApp za kawaida wakikosa program hiyo.

Aidha kulingana na taarifa yao waliyoitoa siku chaze zilizopita ni kuwa program hiyo itawasaidia watumiaji wake kuunganisha akaunti zao mbalimbali za mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook, Twitter (X), Linked, YouTube na mingineyo.

Ili kulinda taarifa binafsi za mtu watumiaji wanaweza kuwaficha akaunti zao kwa watu ambao hawataki wajue kuhusiana na mitandao yao ya kijamii, hivyo basi utaweza kukamilisha hilo kwa kufanya setting katika upande wa WhatsApp yako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags