Kati ya vitu vinavyohesabika kama mafanikio kwa mwanamuziki ni utoaji wa albamu. Kwani huonesha ukomavu wake kwenye gemu.
Kawaida albamu, EP na mixtape zinatofautishwa kwa idadi ya nyimbo, dakika za nyimbo zote kwa ujumla na lengo kuu la kimaudhui. Inaelezwa kuwa albamu inatakiwa iwe na nyimbo kuanzia nane na kuendelea, ambazo kwa ujumla zinakuwa na dakika kati ya 30 hadi 80.
Muhimu zaidi albamu inapaswa kuwa na mtiririko wa kimaudhui unaoshabihiana toka wimbo wa kwanza hadi mwisho. Msikilizaji anatakiwa kuwa kama anasoma kitabu kinachoelezea jambo fulani kuanzia ukurasa wa mwanzo hadi wa mwisho.
Kwenye kiwanda cha muziki Bongo kila mwaka baadhi ya wasanii wamekuwa kutoa albamu mbalimbali kwa ajili ya kuburudisha mashabiki wao. Hawa ndiyo wasanii wenye albamu nyingi zaidi Bongo.
Mr. II Sugu (10)
Ndiye anaongoza kuwa na albamu nyingi Bongo, ambazo ni Ni Mimi (1995), Ndani ya Bongo (1996), Niite Mister II (1998), Nje ya Bongo (1999), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001), Itikadi (2002), Sugu (2004), Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006)na VETO (2009)
Lady Jaydee (9)
Dada Mkuu anashika namba mbili kuwa na albamu nyingi Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), Nothing But The Truth (2013), Woman (2017), 20 (2021) na ile ya ushirikiano akiwa na Rama Madee Love Sentence (2023)
Nikki Mbishi (8)
Mkali huyu wa Hip-hop anayeshikilia rekodi ya kuwa na albamu nyingi zaidi kati ya wasanii wa muziki huo na akishika namba tatu kati wa wasanii Bongo wenye albamu nyingi tayari ameachia Sauti ya Jogoo (2011), Malcom XI (2013), Ufunuo wa Unju Bin Unuq (2015), Sam Magoli (2018), Welcome to Gamboshi (2022), K.I.G.U (2024), Katiba Mpya (2024) na Spana za Unju (2024).
Aidha wasanii wengine waliopo kwenye chati hii ni Soggy Doggy (5), Juma Nature (5) Harmonize (5), Professor Jay (4), Mh. Temba (3), Fid Q (3), Diamond Platnumz (3), Alikiba (3), Barnaba (3), Navy Kenzo (3) na wengineo.
Leave a Reply