Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali tukio hilo la kuomba radhi lilikuwa likifanyika kila ifikapo December 31 lengo kuu likiwa ni kuanza mwaka unaofuata kwa Amani.

Katika siku hiyo wanawake walitakiwa kujitokeza kuomba msamaha hata kama hakuwa na kosa ili familia ianze mwaka mpya katika hali ya Amani na utulivu. Msamaha huo mara nyingi ulifanyika ndani ya nyumba au katika mikusanyiko ya kifamilia, hasa wakati wa sherehe za mwaka mpya.
Aidha kwenye baadhi ya maeneo, wanawake waliandika barua za msamaha au waliandaa milo maalum kwa waume zao kama njia ya kuonesha toba na kushukuru kwa mwaka uliopita.
Hata hivyo, kuanzia katikati ya karne ya 20, mtazamo huo ulianza kupingwa na wanaharakati wa haki za wanawake waliodai kuwa tamaduni hizo zilikuwa za kibaguzi na zilidhalilisha utu wa mwanamke huku wakisisitiza kuwa msamaha unapaswa kuwa wa pande zote na si jukumu la mwanamke pekee katika familia.
Leave a Reply