Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Zuchu ametoa onyo kwa mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa mwanamke kwa kumtafuta mumewe msanii Diamond Platnumz usiku.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka mtu huyo ambaye jina lake linaanzia na herufi ‘A’ kuacha mara moja kumtafuta mumewe kwani kwasasa ameoa.
“Sielewi kwanini mtu unaweza kumpigia mume wa mtu simu usiku wa manane kwani hujui kama ana mke?. Kama unajua jina lako linaanzia na ‘A’ naona call zako acha kumpigia mume wangu,’’ameandika Zuchu
Ikumbukwe wawili hao walifunga ndoa miezi michache iliyopita taarifa ambayo ilitolewa na Diamond mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kushare picha huku akiachia ujumbe ambao uliacha maswali kwa mashabiki.
Hata hivyo maswali hayo yalijibiwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Kawambwa wakati alipozungumza na Mwananchi Mwezi Juni ambaye alithibitisha kuwafungisha ndoa wawili hao miezi sita iliyopita.
"Kwanini watu wanapenda watu wengine wazini, Diamondi na Zuchu ni kweli nimewafungisha ndoa mimi toka miezi mitano iliyopita, ila hilo swali lako unaloniuliza kuhusu wameachana mimi silifahamu, sababu kama wangekuwa wameachana Diamondi angekuja kuniambia mimi.
"Vile mlivyoona kwenye mitandao ni kweli ndoa wala sio kiki, ila naona watu wengi wameshtushwa na hii habari,maana mmezoea kuwasema sema Diamondi na Zuchu wazini kila kukicha sasa hili jambo la kheri lishangilieni na kuliombea kheri"amesema Warid

Leave a Reply