Burna Boy kutoana jasho na ma-rapa wakubwa tuzo za BET Hip Hop

Burna Boy kutoana jasho na ma-rapa wakubwa tuzo za BET Hip Hop

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Burna Boy anatarajia kutoana jasho na ma-rapa wakubwa kutoka Marekani katika tuzo za BET Hip Hop za mwaka 2024.

Kupitia tuzo hizo zinazotarajia kutolewa Oktoba mwaka huu Burna ambaye ametauliwa kuwania katika kipengele cha ‘Best Live Performance’ atachuana na wasanii maarufu kama Cardi B, Nicki Minaj, Kendrick Lamar, Travis Scott, Drake, Megan Thee Stallion, Missy Elliott, Busta Rhymes, na GloRilla.

Mkali huyo wa Afrobeat ataungana na msanii mwezake Odumodublvck ambaye ameteuliwa kuwania katika kipengele cha ‘Best International Flow’ huku Burna akiwa msanii pekee kutoka Afrika jina lake kutanjwa kwenye kipengele hicho ambacho kimekuwa kikishikiliwa na wasanii wa hip hop wakubwa.

Aidha katika orodha hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyoisha msanii anayeongoza kuwa na teuzi nyingi ni ‘rapa’ Megan Thee Stallion ambaye ametajwa kwenye vipengele 12 na wapili akiwa Kendrick Lamar akitanjwa kuwania tuzo kwenye vipengele 11.

Tuzo za BET Hip Hop Awards zinatarajiwa kutolewa Oktoba 15, 2024 Las Vegas, Nevada.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags