Davido matatani kufungiwa kutofanya show Nigeria

Davido matatani kufungiwa kutofanya show Nigeria

Nyota wa Afrobeats Davido amedokeza kuwa onesho lake linalotarajiwa kufanyika mwezi Disemba nchini Nigeria linatishiwa kufutwa kufuatia na msanii huyo kutoa maneno yenye utata kuhusu uchumi wa nchi hiyo.

Utakumbuka kuwa wiki chache zilizopita Davido alieleza kuwa uchumi wa nchi hiyo upo katika hali mbaya kauli ambayo ilizua mabishano baina ya Wanigeria na nchi nyingine.

Wakati marumbano hayo yakiendelea katika mitandao ya kijamii Davido kupitia moja ya mahojiano ya hivi karibuni alifichua jambo jingine kwa kudai kuwa anapokea vitisho vya kusitishiwa kwa show yake inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Lagos.

“Wanasema wataizuia shoo yangu kwa sababu ya maneno niliyosema kwenye mahojiano yangu nadhani sintofanya shoo hiyo nchini Nigeria” aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags