Diamond, Nandy wapiga Mtonyo mrefu Kenya

Diamond, Nandy wapiga Mtonyo mrefu Kenya

Jumamosi ya jana Desemba 21, 2024 wasanii Diamond Platnumz na Nandy walipata show ya kutumbuiza kwenye harusi nchini Kenya, performance ambayo inaelezwa kuwa ya muda mfupi lakini yenye pesa nyingi.

Kupitia kurasa za Instagram za wasanii hao walichapisha malipo waliyoyapata kwenye harusi hiyo Diamond aliandika amelipwa $ 1 million sawa na Sh 2.3 bilioni 2.3 huku Nandy akieleza kulipwa 827 milioni ambapo aliandika "Getting paid $ 350K is noJoke".

Harusi hiyo ya kifahari ilikuwa ya mtoto wa mfanyabiashara mkubwa kutokea Mombasa, ambaye kijana wake Zakir Khosla ndio alikuwa anaoa.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na waheshimiwa mbalimbali akiwemo Rais wa nchi hiyo William Ruto.

Harusi inawaweka Nandy na Diamond kuwa wasanii vinara kutokea Afrika Mashariki kulipwa kiasi kikubwa cha pesa kwenye utumbuizaji wa Harusini.

Hii inatafsiri wasanii wa Bongo Fleva wanaendelea kupanda thamani kila siku. Utakumbuka hivi karibuni Diamond alipata show nchini humo kwenye Tamasha la Furaha City Festival ambapo alilipwa kiasi cha 400 milioni .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags