Moja ya wimbo unaotamba katika mitandao ya kijamii ikiwemo Tiktok na Instagram ni wa rapa kutoka Marekani Nicki Minaj ‘High School’ wimbo ambao amemshirikisha Lil Wayne uliyoachiwa mwaka 2012.
Wimbo huo umerudi tena katika chati za muziki kufuatia na pozi alilokaa msanii huyo mwanzoni mwa video ya wimbo ambapo mashabiki kutoka pande zote za dunia wamechukua pozi hilo na kufanya challenge ambapo ndani ya siku nne zaidi ya watumiaji wa Tiktik 100k wameshafanya challenge hiyo.
‘High School’ wimbo ambao unapatikana katika Album ya Nicki iitwayo ‘Pink Friday: Roman Reloaded – The Re-Up’ iliyoachiwa mwaka 2012 ikiwa na ngoma 16.
Mafanikio ya ‘High School’
Wimbo huo ulishika nafasi ya 64 kwenye chati ya Billboard Hot 100. Pia ulifika nafasi ya 15 kwenye chati ya Hot Rap Songs na nafasi ya 20 kwenye chati ya Hot R&B/Hip-Hop Songs, mbali na hilo lakini pia ulivuka boda ukiingia kwenye chati ya Uingereza (UK Singles Chart) na kufika nafasi ya 31.
Katika mauzo, wimbo huu umetunukiwa Platinum mara mbili nchini Marekani, na Silver (Fedha) nchini Uingereza kwa mafanikio yake ya kibiashara.
Wimbo huo uliandikwa na Nicki Minaj, Lil Wayne, Matthew Samuels, na Tyler Williams, huku producer akiwa Boi-1da na T-Minus ambao ni watayarishaji maarufu wa muziki wa hip hop.

Leave a Reply