Hii hapa filamu iliyofilisi watayarishaji na waigizaji

Hii hapa filamu iliyofilisi watayarishaji na waigizaji

Mwaka 1963 dunia iliipokea filamu kubwa ya Cleopatra ambayo iliwavuruga wengi kutokana na urembo wa muhusika mkuu Elizabeth Taylor.

Licha ya kupokelewa na watu wengi kampuni ya 20th Century Fox na waigizaji wake walidaiwa kufilisika kutokana na filamu hiyo kuwa na gharama kubwa katika uandaaji wake.

Awali filamu ya Cleopatra ilipangwa kutumia dola milioni 2 lakini mambo yalienda kombo kutokana na kukumbana na changamoto mbalimbali hadi kupelekea filamu hiyo kutumia zaidi ya dola milioni 44.

Hali ya kifedha ya 20th Century Fox ilianza kutetereka baada ya kuhamishwa kwa seti kutoka Ungereza hadi Roma, Itali katika studio ya Cinecittà. Uhamisho huo ulisababisha kupotea kwa zaidi ya dola milioni 7.

Aidha filamu hiyo ilifanikiwa kuingiza zaidi ya dola milioni 57 duniani kote lakini mapato hayo hayakurudisha gharama zilizotumika. Umaarufu wake mkubwa haukuweza kufidia hasara kwa wakati huo lakini ulisaidia kampuni hiyo kurudi katika nafasi yake taratibu.

Mwaka 1961, baada ya filamu hiyo kusababisha hasara kubwa ya kifedha, kampuni ya 20th Century Fox iliuza takribani ekari 180 ya ardhi ambayo iliwekwa kwa ajili ya kutengeneza studio kubwa maeneo ya Beverly Hills/West Los Angeles, ardhi hiyo iliuzwa kwa William Zeckendorf na kampuni ya Aluminum Co. of America (Alcoa), kwa dola milioni 54.

Hata hivyo baada ya mradi huo kuwepo na hasara kifedha lakini pia ulilazimika kusitisha miradi mingi ya filamu, ikiwa ni pamoja na vipindi vya sinema vilivyokuwa vikirushwa kwenye televisheni, filamu mpya kufutwa kabla ya kurekodiwa pamoja na kuondoa wafanyakazi katika vitengo mbalimbali ikiwa pamoja na wabunifu, maandalizi na watu wa masoko.




Hali ya 20th Century Fox kwasasa

Mwaka 2020, kampuni ya 20th Century Fox iliuzwa rasmi kwa The Walt Disney Company kwa takribani dola bilioni 71.3 ambapo Disney ilifanikiwa kumiliki sehemu kubwa ya mali za Fox, ikiwemo studio za filamu, vipindi vya runinga, franchise za filamu, na hakimiliki.

Jina la kampuni lilibadilishwa kutoka '20th Century Fox' na kuwa '20th Century Studios' huku ikifanikiwa kutoa filamu kama Avatar: The Way of Water (2022), The Creator (2023), Free Guy (2021), Planet of the Apes na nyinginezo.


Elizabeth Taylor kupendelewa

Licha ya kuwa Elizabeth Taylor alikuwa muhusika pendwa katika filamu ya Cleopatra pia aliweka historia kwa kuwa mwigizaji wa kwanza duniani kulipwa dola milioni 1 kwa filamu moja.

Hilo lilikuwa sehemu ya mkataba wake wa kipekee na 20th Century Fox, ambao pia ulimpa asilimia ya mapato ya filamu kupitia kipengele cha 'profit participation' huku malipo yake yakiendelea kuongezeka kufikia hadi dola milioni 7.

Lakini kwa upande wa waigizaji wengine, filamu hiyo ilizua migogoro ya kifedha kutokana na ucheleweshwaji wa malipo uliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Hata hivyo wasanii waliungana kuifungulia kesi kampuni ya 20th Century Fox kutowalipa fedha zao, huku wakimlalamikia Taylor kupendelewa zaidi. Kufuatia na hilo wasanii walijikuta wakifilisika kutokana na kutosaini mikataba mingine ya nje wakiamini katika filamu hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags