Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone leo Februari 19,2025 anatarajia kufanyiwa upasuaji wa kongosho nchini Marekani katika Hospitali ya Allina Health Mercy iliyopo Coon Rapids, Minnesota.
Mwimbaji huyo ambaye saa chache zijazo atafanyiwa upasuaji huo mkubwa. Kwa mara ya kwanza Desemba, 2024, mwanaye aitwaye Abba Marcus aliweka wazi kuwa baba yake anasumbuliwa na maradhi hayo yaliyosababishwa na uraibu wa pombe kali kwa muda mrefu.
"Natamani kila mmoja afahamu kuwa kama baba yangu ataendelea na unywaji wa pombe kwa mujibu wa madaktari hatochukua miaka zaidi ya miwili kuishi. Hii inaniumiza sana kwa sababu huyu ndiyo baba yangu niliyemfahamu kwa muda wangu wa maisha," alisema Marcus.
Hata hivyo baada ya taarifa hiyo ya mtoto wake Waziri wa Nchi Vijana na Masuala ya Watoto nchini Uganda Balaam Barugahara, alipokea agizo la Rais Yoweri Museveni la kutaka msanii huyo apelekwe Marekani kwa ajili ya matibabu.
Tangu kupelekwa kwake Marekani kwa ajili ya kupatiwa matibabu, sasa anatarajia kufanyiwa upasuaji huo kwa ajili ya kuirudisha afya yake kwenye hali ya kawaida.
Utakumbuka Chameleone alitamba na ngoma kama vile Valu Valu, Tubonge, Badilisha, Shida za Dunia, Jamila na Wale Wale,

Leave a Reply