Kanye Aonesha Mashaka Malezi Ya Watoto Wake

Kanye Aonesha Mashaka Malezi Ya Watoto Wake

Mwanamuziki na mfanyabiashara Kanye West ameonesha kuwa na wasiwasi katika malezi ya watoto wake ambao wanalelewa katika familia ya aliyekuwa mke wake Kim, ‘The Kardashian Family’.

Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa X ameeleza kuwa siku ya kifo cha gwiji wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant, mwaka 2020 alitembelea nyumbani kwa Kylie Jenner. Ndugu wa Kim Kardashian nyumbani hapo aliona vitu visivyo vizuri kwa malezi ya watoto.

“Nahitaji mpango wa kutumia haki zangu kuhusu watoto wangu. Nimeweza kuelewa mambo mengi lakini hili bado sijalielewa. Siku ambayo Kobe alikufa, wote tulienda kwenye nyumba ya Kylie, na pale karibu na kochi sebuleni kulikuwa na majarida ya zamani ya Playboy yaliyowekwa kwa makusudi karibu na sehemu yoyote ambayo mtoto angeweza kuyafikia na kila mtoto aliyekuwepo pale alikuwa na damu ya Kiafrika kiasi.

“Ninyi mnajua hilo linamaanisha nini. Kwa nini lilikuwa hivyo. Na nani aliyehusika. Wimbo wa 'Cousin' hunikumbusha jambo hilo. Mimi kama baba, nilitamani kubadilisha hilo kwa ajili ya watoto wangu,”ameandika Kanye

Utakumbuka Kanye West ana watoto wa nne na Kim Kardashian ambao ni North West, Saint West, Chicago West na Psalm West watoto wawili wakiwapata kwa kupandikiza mbegu kwa mama mwingine ‘surrogate’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags