Nguli katika muziki wa Taarabu, Khadija Kopa amejitosa tena katika muziki wa Singeli ambapo jana sauti yake ilisikika katika ngoma ya ‘Mama’ akishirikishwa na mkali wa Singeli Barobaro.
Akizungumza na Mwananchi Barobaro ameeleza kuwa hakukua na ugumu wa kufanya kazi na Kopa.
“Mimi ndio nilimtafuta ili niweze kufanya naye ngoma lakini ni mtu ambaye anapenda ninachokifanya kwa hiyo haikutia ugumu wowote mimi kufanya naye kazi, ni mtu anayependa ninachokifanya kwa hiyo hata nilivyomwambia tufanye project ya pamoja alikubali na nyimbo yake pendwa ilikuwa ni hiyo."
Wakati tunaingia studio maelekezo hayakuwa mengi kwa sababu yeye ni mkongwe na ana uzoefu na kazi yake, yaani maelekezo yalikuwa machache ni mtu ambaye ameonekana kuwa na uzoefu kwa sababu anazunguka sana na wasanii wa singeli na anaona wanachokifanya kwa hiyo maelekezo yalikuwa madogo madogo tuu ya kisingeli lakini kwenye kurekodi hakukuwa na shida yoyote,”amesema
Akizungumza kuhusu kufanya naye kolabo nyingine ya Singeli Barobaro ameeleza kuwa tayari wamekubaliana kufanya kazi nyingine na kilichobaki ni kuingia studio.
“Project nyingine zipo lakini main ilikuwa ni hii ‘Mama’ kama unavyojua mwanzo kuna wasanii walikuwa wanaitumia sana kuimba kwenye majukwaa ikiwa sio mali yao kwa hiyo yeye bimkubwa akawa ananiuliza mbona hutoi ile project basi nikamuomba tuanze kwanza na hii, project nyingine ipo ya pamoja japo hatujaifanya bado ila anaijua.
Haikuwa na ugumu wowote kufanya naye hii kazi wala hakuwa na kipengele alinipa ahadi nikaenda lakini sikumkuta ila aliniomba ni msubiri ili tuweze kufanya hiyo kazi, unaona ni jinsi gani inamanisha alikuwa tayari na kile kitu na hakutaka kunizungusha, alivyokuja tukaifanya pale akaniuliza kama nimeridhika na kama sijaridhika turudie, bimkubwa ni mtu poa sana huwezi amini hii project tumeifanya palepale kwake,”amesema
Sababu Kopa kupenda muziki wa Singeli
“Msanii wa taarabu kuipenda singeli mfano Khadija Kopa alichokifanya ni kutaka tu kuleta ladha mpya, kuna watu wataarabu walikuwa hawapendi Singeli wanasikiliza Taarabu lakini wakisikia muziki wa singeli umeimbwa na Khadija Kopa naamini watu wa taarabu nao watakuja huku ukizingatia ni muziki ambao unakubalika sana ndani nan je ya nchi kwasasa,”amesema Barobaro.
Aidha ameongezea kwa kueleza kuwa kufanya kwake kolabo ya singeli na Kopa ni mafanikio makubwa kwake huku akiwataka mashabiki kuendelea kumsapoti kwani amekuwa akisikiliza ushauri wao kila siku huku akiweka wazi kuja na kolabo nyingine kubwa kutoka kwa mastaa wenye majina.
Hii sio kolabo ya kwanza ya Singeli kwa nguli huyo wa taarabu miaka michache nyuma aliwahi kufanya wimbo wa singeli uitwao ‘Mshamba wa Kamera’ akishirikishwa na Mzee wa Bwax.

Leave a Reply