Video Chafu Za Diddy Zaoneshwa Mahakamani

Video Chafu Za Diddy Zaoneshwa Mahakamani

Wakati kesi ya rapa kutoka Marekani ikiendelea kuunguruma mahakamani, jana Jumatatu Juni 16, 2025, majaji walishuhudia vipande vya video zinazodaiwa kuwa za Party za rapa huyo zilizokuwa zikifanyika kuanzia miaka 1990 mpaka 2020.

Kwa mujibu wa ripoti zilizototelewa na TMZ, utazamaji wa video hiyo ulitokea wakati wa ushahidi wa wakala maalumu wa Idara ya haki ambapo katika ushuhuda huo, wakala huyo alifichua orodha ya hoteli ambazo inadaiwa kuwa matukio ya ajabu yalitokea huku akionesha video tatu na kila moja ikiwa na urefu wa dakika 11 hadi 12.

Chumba cha mahakama kilinyamazishwa wakati wa kutazamwa, na sauti za vilio na zaidi zilisikika kupitia vifaa maalum vya masikioni vya mahakimu.

Aidha kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya mahakama, upande wa mashtaka unakaribia kukamilisha ushahidi wake kabla ya wiki ya sita kuisha huku ikiwa na maana kuwa muda si mrefu upande wa Diddy utaanza kuwasilisha hoja zake.

Mpaka kufikia sasa zaidi ya mashahidi 18 tayari wametoa ushahidi wao akiwemo aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Diddy, Cassie Ventura (Cassie), Jane (Ex wa Diddy), Kid Cudi, Mia, Capricorn Clark, Kerry Morgan, Bryana Bongolan na wengineo.

Diddy anakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, njama ya kihalifu (racketeering), na usafirishaji kwa lengo la kushiriki katika ukahaba. Amekana mashitaka yote na endapo atapatikana na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Utakumbuka Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn. Kesi yake ilianza kuzikilizwa Mei 5,2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags