kutoka Darassa hadi Leornado

kutoka Darassa hadi Leornado

KUTOKA DARASSA HADI LEONARDO

"...255 Champion Boy niite Mbwana Samatta, haaa..." Dude la kibabe sana. Linaanza kibingwa, linaisha kindava. 'Biti' ya kikatili kama isaundi traki' ya 'muvi' la kimafia. Lazima ukae.

Alikuwa yeye tu kwa kipindi kirefu. Aliwafunika wanamuziki wote mpaka mashabiki wao. Miaka mingi ilipita bila wimbo wa kutikisa nchi kutoka. Hadi Darassa alipokuja na "Muziki".

Alishitua watu na wasanii wenzake. Kadiri muda ulivyokwenda. Na ndivyo vituko vilizidi kupitia pini hilo. Achana na yule dereva wa Singida. Aliyeachia usukani, gari ikiwa kasi.

Yeye na abiria wake wakipandisha ile mizuka na wimbo wa Darassa. Totoz mitandaoni zilijirekodi zikicheza pini lile. Ilivutia sana. Hata mistari yake ilogeuka misemo mitaani.

Wimbo ulipendwa na watoto, wazee na zaidi vijana. Kilichotia chumvi zaidi ni watoto wazuri wa mjini kujirekodi. Wakiucheza na kutupia mitandaoni. Ilizidi kunogesha utamu wa wimbo.

Ungetamani kuona Lulu akiucheza wimbo huo. Kwa namna ya pekee akifuatisha 'biti' na mistari ya Darassa kwa maringo. Ungedata na Jokate. Na yeye alijirekodi kwa kujidekesha.

Alikiwa kama mtoto anayefundishwa kuucheza. Ilitia raha kumtazama Jojo.
Na kuna binti mzuri zaidi na mdogo zaidi. Alijirekodi kwenye duka la nguo. Kila kidume kilitamani kumfahamu.

Umbile lake na namna alivyofuatisha wimbo. Iliwachanganya akili. Hasa pale anaposema "Waote mapembe waongezee mkia". Kila binadamu mchizi muziki alidata na Darassa.

Ndiye pekee aliyepita katikati ya msitu wa Mondi na Kiba. Akapasua na kuwaacha wasiamini kinachotokea.

Ikawa ngumu watu kusikiliza wimbo mpya. Likawa pigo kwa Dimpoz na "Kajiandae" akiwa na Kiba.

Rich Mavoko na "Kokoro" akiwa na Mond. FA na "Dume suruali" akiwa na Vanessa. Wote nyimbo zao zilizimwa ghafla. Ulikuwa wimbo wa taifa. Ni lazima wangenyoosha mikono juu.

Na wenye roho nyepesi walisusa na game lenyewe la muziki. Ujio wake kama Ngwair na "Mikasi". Ferouz na "Starehe". Pro. Jay na "Ndiyo Mzee". Nature na "Sitaki demu". King Kina na Cinderela.

Ulipita muda mrefu bila kutoka wimbo wa kushitua watu. Kusambaa kwenye mioyo ya watu rika zote. Hadi balaa la Darassa kutua kama bomu la nyuklia. Ulikuwa ni ukatili kwa wenzake.

Ni kama Inspector Haroun na "Mtoto wa geti kali". Tulimsikiliza Inspector kila wakati kuliko taarifa ya habari. Ni kama "Kikulacho" na Mr Nice. Kama "Zeze" na TID Mnyama. Nomaa!

Darassa baada ya wimbo wake huo. Akachoshwa na safari za kwenda kwenye shoo. Alikerwa na simu za mapromota na waandishi. Akaumizwa bega kwa 'hagi' za 'fansi' na totoz.

Unadhani wimbo wa "Muziki" ulikuwa bora kuliko nyimbo zote za Darassa? Unaweza kuwa ndo wimbo ambao hakutumia akili na muda mwingi sana kuandaa. Ni wakati tu, ukifika hakuna wa kuzuia.

Watu walichoka na mbio za wale watu wawili tu kila siku. Masikio yalitaka kitu kipya. Ndiyo maana kila kona ikawa ni Darassa tu. Lakini leo unamsikia? Rahisi kumsikia Leonardo na Mwaisa kuliko yeye.

Yupo na anafanya vizuri kuliko hata zamani. Mr Burudani kaendelea kuwa noma zaidi. Lakini hayupo masikioni mwa watu kama awali. Watu hawataki muziki? Hapana, kuna tatizo la ufundi kwenye bongo za Wabongo.

Unapowaona kina Mondi, Konde Boy, King Kiba na wengineo. Wakiendelea kukimbiza kwenye 'meinistrimu'. 'Jasti puti samu rispekti kwao". Wanapigana vita ngumu sana. Darassa yupo lakini siyo kama yule.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags