Maandalizi Kuelekea Harusi Ya Jux Na Priscy, Kesho

Maandalizi Kuelekea Harusi Ya Jux Na Priscy, Kesho


Tazama maandalizi kuelekea sherehe ya Jux na mke wake Priscilla inayotarajiwa kufanyika kesho Mei 28,2025 katika ukumbi wa Warehouse jijini Dar es Salaam.

Utakumbuka kuwa baada ya kumaliza kufanya sherehe nchini Nigeria na kuzua gumzo katika mitandao ya kijamii iliyofanyika April 17 na 19, 2025 jijini Lagos na sasa wawili hao wanaenda kufanya balaa lingine Bongo ambayo sherehe hiyo itakuwa ya mwisho.

Wawili hao walifunga ndoa Februari 7,2025 ndoa ambayo ilihudhuriwa na na watu wachache wakiwemo ndugu wa karibu pamoja na wasanii kama vile Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Abba, Ommy Dimpoz na wengine.

https://www.instagram.com/reel/DKJq_dmNnXr/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Mahusiano ya Jux na Priscy yalianza mapema Agosti 2024 huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandano ya kijamii ya ndani na nje ya Tanzania baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.

Ikumbukwe kabla ya Jux kuwa kwenye mahusiano na Priscilla, alikuwa na Karen Bujulu. Priscilla Ajoke Ojo alionekana kwa mara ya kwanza na Jux July 19,2024 kwenye moja ya kumbi za starehe zilizopo jijini Dar es salaam. Na hii inakuwa ndoa ya kwanza kwa wapenzi hao wawili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags