Mambo ya kuzingatia kabla ya kujiremba

Mambo ya kuzingatia kabla ya kujiremba

Haya haya, wale watu wangu wa fashion kujeni hapa, nina kikao na nyie. Leo nitazungumza na wadada na warembo wote ambao wanapenda kujiremba na kuwa na mwonekano mzuri.

Kujiremba sio kupaka make up tu bali mwonekano wako wote kuanzia juu mpaka chini. Leo nimekuja na mbinu au mambo ya kuzingatia kabla ya kujiremba ili usiende kuwa kichekesho uendako, kama ni kwenye harusi au mtoko tu wa kawaida.

Vitu vya kuzingatia kabla ya kujiremba


  • Cha kwanza ni kujua ngozi yako. Ngozi ya mwanamke ni bora ‘sensitive’ sana na inatakiwa ipakwe aina ya mafuta au lotion yenye virutubisho kulingana na aina ya ngozi.

Kuna wanawake wenye ngozi ya mafuta ‘Oily Skin,’ kuna wenye ngozi mchanganyiko na kuna wale wenye ngozi kavu (Dry Skin).

Ni vyema mwanamke kujua aina ya ngozi yake ili ujue aina ya product ya ngozi unayopaswa kutumia na siyo kwa sababu umemuona mwenzio anapaka aina fulani ya losheni na wewe unakimbilia kununua. 

Kingine hapa katika ngozi ni kuangalia foundation ambayo haijakaa muda mrefu na utumie rangi yako, sio foundation ya mtu mweusi unapaka wewe mtu mweupe au maji ya kunde

 

  • Kope

Kabla ya kwenda saloon kujiremba lazima uangalie aina ya kope ambazo utazimudu maana kuna aina za kope mbali mbali: ndefu, fupi na za kawaida kabisa, so angalia ni ipi itakufaa na rangi gani ya kupaka kwenye kope zako, usipake tuu kwa kuona msanii maarufu kapaka na wewe utajua utapendeza, shoga yangu utachekesha jamii.

 

  • Rangi ya mdomo

Hapa sasa ndo kuna matatizo kama yote japo kuwa ndo urembo ambao unawapendeza wanawake wengi wanapopaka rangi ya mdomo, kitu watu ambacho hawakifahamu kwamba tunatofautiana sana midomo au lips, hata kwenye rangi za midomo pia inakwenda sawa na lips zako. Usipake tuu kisa rafiki yako kapaka kapendeza hapana, tafuta ushauri ili ujue lips zako au mdomo wako unapendeza rangi ipi ya mdomo.

 

  • Kucha

Eeeeeeh! Hapa sasa kwenye kucha jamani jamani, sawa hatukatai ni urembo lakini mwanamke huwezi kuweka kucha ndefu za kubandika mpaka kushindwa kula ama kufua kwasababu ya urefu wa kucha. Wengine wenzangu na mie wazee wa kung’ata kucha yaani unatafuna kucha mpaka inakuwa haina mvuto binti. Kama kweli wewe ni mrembo na una mtoko usiku, basi weka kucha zako vizuri hata mtu akikushika mkono aseme woow.

Na kwa wale ambao ni wapenzi wa kula kucha, jambo la kufanya ni kutafuta wataalamu ili uweze kupata suluhisho la tatizo hilo, kama kucha zimepata fangasi ili kupata dawa na kutibu kabisa.

 

  • Marashi/ perfume/ oud

Manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini ni muhimu kwa wanawake lakini ni vyema nikaweka angalizo. Haipendezi kwa mwanamke anayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine. Ni vyema wanawake wakajipulizia marashi yenye staha na yasiyokera.

  • Rangi ya nguo na viatu

Sasa hili jipu kabisa utakuta mtu kavaa nguo ambayo haiendani na viatu alivyovivaa, so ukitaka kutokelezea ama kudamshi kama waswahili wanavyosema, basi binti jua kujipangilia kuanzia viatu mpaka nguo, itakusaidia kukupa muonekano mzuri uendako kama kwenye shughuli, party au mtoko wa usiku.

  • Accessories/ hereni bangili

Hahaahha! Make hapa kwanza ncheke sio kwa mazuri lakini kuna watu wanachekesha sana jamani, yaani unakutana na mdada mrembo kila kitu kimekaa mahali pake lakini sasa mkononi kajaza mikacha, bangili, sijui vidani yaani tafrani, kingine cha kuzingatia ni kupangilia kitu gani kikae kwenye mkono wako na kipi kisikae sio unajijaza mivitu isio ya maana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags