Manara: Siwezi kufanya kiki za mapenzi, msimamo wangu ndio huo

Manara: Siwezi kufanya kiki za mapenzi, msimamo wangu ndio huo

Unaweza kusema haikuwa bahati kwa waliokuwa wakipendanao, Haji Manara na mwigizaji Zaiylissa. Baada ya wawili hao kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii wakionesha penzi lao si penzi tena bali ni majanga huku Manara akisema hiyo siyo kiki bali ndiyo uhalisia wa kinachoendelea baina yao.

Miezi michache nyuma zilianza tetesi kwenye mitandao ya kijamii zikihusisha wawili hao kuwa hawako katika maelewano, lakini Haji Manara alikanusha hilo na baadaye wakaendelea kuonekana pamoja.

Hata hivyo awamu hii baada ya tetesi hizo mambo yamekuja kivingine, baada ya mwigizaji Zaiylissa kuchapisha jumbe mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii akidai kuchoshwa na ndoa yake na Manara huku akisisitiza amekuwa akihangaika kwa muda mrefu kutaka talaka yake bila mafanikio.

"Imetosha sasa nimechoka kupretend. Sasa acha tuvuane nguo kama ulivyozoea mtoto wa dada yangu amekuja kukaa likizo kwa mapenzi. Na muda wake wa kuondoka ulivyofika ulimzuia. Kumbe ulikuwa unamtongoza shame on you!(aibu juu yako) ulikuwa na kazi ya kumshika shika binti mdogo wa under 18! Sasa round hii umegusa pabaya.

"Umezoea kulala na house girl sasa ukaona uhamie kwa binti yangu loh. Unamtumia mtoto Sh 50,000 vyako akiwa shule ili umlaghai kwa taarifa yako tuna ushahidi wote. Na driver wako pia anajua kila kitu na tumeambiwa hatutakukalia kimya, kila nikiomba talaka yangu hutaki kunipa. Unagombana na mimi unamwambia kijana wako arekodi. Sasa round hii sicheki, ushazoea kudhalilishana," aliandika Zaiylissa.

Hiyo ni kati ya jumbe alizochapisha Zaiyllisa kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumfanya Haji Manara ajibu.

"Mtoto wangu na wazazi wangu wapo juu ya kila kitu, unamnyanyasa mwanangu hata kwa chakula halafu ulitaka tuendelee kuishi ndani kwangu? Mwanangu wa kumzaa umnyime hadi chakula? Yote naweza kusamehe ila kwa mwanangu na familia yangu big no. Siwezi kustahmili," alijibu Manara.

Baada ya hayo yote, Manara amezungumza na Mwananchi na kusema kila kinachoendelea ndiyo msimamo wake.

"Mimi sina muda wa kuendelea kujibizana, nilichokisema ndiyo msimamo wangu. Muacheni huyo anayeendelea kuandika. Kuhusu kutoa takala no komenti, lakini siwezi kufanya kiki, kwa nini nifanye kiki ya kuachana, hayo mambo mimi sinaga," Manara ameiambia Mwananchi.

Mwananchi ilipomtafuta Zaiylissa kuzungumzia hilo, aliomba kutumiwa ujumbe na hata alipotumiwa hakujibu.

Utakumbuka ndoa ya wawili hao ilifungwa Januari 24,2024 huku ikiwa ni ndoa ya sita kwa Manara na ya pili kwa Zaiylissa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags