Mandonga: ndoige ni kama palapanda haimuachi mtu salama

Mandonga: ndoige ni kama palapanda haimuachi mtu salama

Hahahhaa! Make hapa kwanza nchekee, sio powa kabisa yule Mandonga mtu kazi bwana amefunguka na kusema kuwa safari hii amekuja kivingine na kutambulisha ngumi yake mpya inaitwa ndoige yaani hiyo ukikutana nayo haikuachi salama.

Mandonga ameyasema hayo kupitia hamojiano yake na moja ya chombo cha habari na kusema kubwa “kuna ngumi ya kigeni ambayo watanzania wengi bado hawajaijua inaitwa ndoige yaani ukiend kushoto unayo ukirudi kulia unayo na ukienda dukani kununua vocha unakutana nayo mgongoni, yaani hii ngumi ni kama palapanda haimuachi mtu salama” amesema Mandonga mtu kazi

Bwana bwana akamalizia na kamsemo kale ambako kametrend sana katika mitandao ya kijami akisema “Ukinipiga ni kama nimekupiga na nikikupiga nimekupiga tuu mandonga mtu kazi” amesema Karim Mandonga

Nyie nyie embu kujeni hapa wanangu sana mdondoshe komenti zenu je Mtu kazi safari hii atachomoka na ngumi yake mpya au atapigwa kama kawaida yake?.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags