Mauzo ngoma za Diddy yapanda

Mauzo ngoma za Diddy yapanda

Kufuatia kukamatwa kwa mwanamuziki Sean “Diddy” Combs wiki iliyopita imeripotiwa kuwa mauzo ya nyimbo zake yamepanda na kupata ongezeko kubwa la wasikilizaji katika kazi zake kupitia mitandao ya kuuzia muziki.

Kwa mujibu wa ABC News, imeeleza kuwa kampuni ya Luminate, inayoshughulika na takwimu katika tasnia ya muziki imeripoti kuwa muziki wa Diddy ulipata ongezeko la wasikilizaji 18.3% kwa wiki iliyoisha.

Sio jambo la kushangaza kuona idadi ya usikilizaji wa muziki ikiongezeka baada ya msanii kukutana na tuhuma flani, utakumbuka mwanamuziki R.Kelly baada ya kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na wasichana wadogo idadi ya usikilizaji wa ngoma zake iliongezeka mara mbili zaidi.

Ukiachilia mbali ongezeko hilo inasemekana huenda Diddy alihisi ipo siku atakamatwa kutokana na sherehe alizokuwa akifanya nyumbani kwake.

Hiyo ni kutokana na moja ya mahojiano yake aliyofanya mwaka 1999 alisikika akieleza kuwa ipo siku polisi watamkamata.

“Mtakuja kusikia kuhusu sherehe zangu, watazifunga. Huenda wakaanza kunikamata, kufuatia na mambo yote ya ajabu tunayoyafanya kwenye sherehe zangu.

“Lakini mimi nafanya sherehe kwa ajili ya kufurahi na kuleta watu pamoja kutoka sehemu zote za maisha.” Alisema Diddy kwenye mwahojiano yake na Entertainment Tonight

Mbali na hayo baadhi ya wanamuziki wakubwa kutoka Marekani wamekuwa wakihusishwa kwenye tuhuma zinazomkabili Diddy lakini kwa upande wa ‘rapa’ Meek Mill amepanga kuwalipa wapelelezi ili kuwafahamu watu wanaolihusisha jina lake na kesi za Combs.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) Meek ameeleza kuwa yupo tayari kutoa kiasi cha dola 100,000 sawa Sh 273 milioni kwa wapelelezi kufanya uchunguzi watu wanaolihushisha jina lake katika kesi zinazomkabili Diddy.

Diddy alikamatwa Jumatatu Septemba 16, na kuzuiwa katika gereza liitwalo ‘The Metropolitan Detention Center (MDC)’ kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags