Video Ya Why Imegharimu Sh 56 Milioni

Video Ya Why Imegharimu Sh 56 Milioni

King Bad, Marioo ametusanua kwamba Video ya wimbo wa ‘Why’ kutoka kwenye album yake ya ‘The Godson’ imeghalimu zaidi ya Sh 56 milioni mpaka kukamilika kwake.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Bad ameweka wazi suala hilo huku akilalamika kuwa kutengeneza video za ndani kuna gharama sana.

“Ila Videos za Indoor ni Expensive sana imagine video yote Tumeshoot ndani lakini Imegharimu zaidi ya M56 Tz’s lakini Nashukuru tumepata Chupa Kali sana,” ameandika Marioo.

Video ya Why ambayo imeachiwa Februari 21,2025 inakuwa ndio video ya kwanza kuachiwa kutoka kwenye album ya ‘The Godson’ iliyotoka Novemba, 29, 2025, ikiwa na mawe 17, ambayo yanasumbua sana kwa sasa kwenye majukwaa ya kusikilizia muziki.

Unaipa asilimia ngapi Video hiyo?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags