Met Gala Ya Bongo Kufanyika Kwenye Sherehe Ya JP2025

Met Gala Ya Bongo Kufanyika Kwenye Sherehe Ya JP2025

Baada ya msanii Jux kuweka wazi kufanya sherehe nyingine Bongo ya reception, na sasa inaelezwa kuwa haitakuwa tuu sherehe bali itakuwa ni maonyesho ya mitindo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Ommy Dimpoz rafiki wa karibu wa Jux ameeleza kuwa Met Gala ya Tanzania itakuwa kwenye sherehe ya harusi ya Jux inayotarajiwa kufanyika Mei 28,2025

“JP2025 niko na seven style sio tu ndoa itakuwa ni Met Gala, Dar es Salaam ni Met Gala jipangeni,”amesema Dimpoz

Sherehe hiyo itakuwa ya mwisho kwa wanandoa Jux na Priscilla ambapo awali walifanya sherehe ya Kitamaduni Nigeria, kufunga ndoa ya Kikristo pamoja na sherehe nyingiza zilizofanyika Tanzania.

Met Gala (Metropolitan Museum of Art Costume Institute Gala) ni hafla ya kifahari ya kila mwaka inayofanyika mjini New York, Marekani, kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya Idara ya Mavazi (Costume Institute) ya jumba la sanaa la Metropolitan Museum of Art.

Na mwaka huu imefanyika Mei 5,2025 huku mastaa mbalimbali wakitokelezea kwa mitindo tofauti tofauti.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags