Misuzulu akanusha kupewa sumu

Misuzulu akanusha kupewa sumu

Mkuu wa ufalme wa kitamaduni wenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Afrika Kusini, Misuzulu Kazwelithini alitoa tamko siku ya jana Jumatatu kuwa yupo salama na akakanusha uvumi kwamba alikuwa amepewa sumu.

Kazwelithini aliambia moja ya chombo cha habari katika mahojiano ya simu kutoka nchi jirani ya Eswatini, ambako anafanyiwa chunguzi wa kimatibabu, kwamba hali yake ya afya ni shwari.

Mwishoni mwa wiki, waziri mkuu wa Zulu mwenye ushawishi mkubwa, Mwanamfalme Mangosuthu Buthelezi, alisema kuwa mfalme huyo amelazwa hospitalini nchini Eswatini baada ya kuugua.

Ingawa Buthelezi alisema kulikuwa na tuhuma kwamba alipewa sumu baada ya kifo kisichotarajiwa cha mmoja wa washauri wake wa karibu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags