Mpango wa Marioo kumuoa Paula upo hivi.. Kajala atajwa

Mpango wa Marioo kumuoa Paula upo hivi.. Kajala atajwa

Mpango wa Marioo kumuoa Paula upo hivi

Paula Paul ambaye ni mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja, na Mzalishaji muziki P Funk Majani, amesema yupo kwenye mpango wa kurudi shule kujiendeleza na masomo huku akikazia kuwa endapo ndoa ikitangulia litakuwa jambo zuri zaidi.

"Nalipokea kwa kawaida jina la Paula sitaki shule, ni fikra zao wenyewe naipotezea. Ninamipango ya kuendelea na shule nasubiri Amara akue. Nataka nikaendelea kusomea fashion kwa sababu ndiyo kitu ambacho napenda nataka kujiendeleza kwenye hilo,"amesema Paula Novemba 25, 2024 wakati akifanyiwa mahojiano na Clouds Media

Aidha amesema endapo Marioo akitaka kumuoa yupo tayari kuolewa kwanza ndiyo asome.

Hata hivyo kwa upande wake Marioo akizungumza katika mahojiano hayo amesema mipango ya kumuoa Paula tayari imefanyika hivyo siku yoyote atatangaza tarehe.

"Sisi tupo kama familia suala la ndoa ni dogo sana, ni kuamua na sheria tumeanza kufuata, mambo ya msingi tumeshafanya imebakia suala la kusema tarehe fulani tunataka kuoana mpango huo upo sababu nampenda, amenizalia mtoto mzuri kwa hiyo kama hitaji lake ni ndoa ni dogo sana barua tulishapeleka,"amesema Marioo

Paula hakuacha kuzungumzia mitazamo ya watu juu ya malezi anayopata kwa mama yake huku wengu wakidai wawili hao hawaheshimiani

"Sisi tuna mipaka hatupo kama watu wanavy






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags