Mtoto wa Davido afariki

Mtoto wa Davido afariki

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari nchini Nigeria vinaripoti kuwa mtoto wa mwanamuziki Davido Adeleke na Mpenzi wake Chioma Rowland amefariki Dunia

Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Ifeanyi Adeleke mwenye umri wa miaka (3) anatajwa kufariki dunia October 31,2022 baada ya kuzama kwenye Swimming Pool nyumbani kwao.

Mapema October 31 Davido alionekana akimfundisha mtoto wake huyo kuogelea huku akimpongeza kwa kuimarika kwenye mchezo huo. Taarifa zinazidi kuripoti kuwa Ifeanyi alizama kwenye maji kwa muda mrefu kabla ya wazazi wake kugundua kutoweka kwa mtoto wao. Baada ya msako kufanyika nyumbani hapo walikuta Ifeanyi akielea kwenye maji.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kuwa walijaribu kumkimbiza hospitali lakini bado haikusaidia kuokoa maisha ya mtoto huyo. Mpaka sasa familia ya Davido haijatoa taarifa yeyote rasmi ya uwepo wa tukio hilo.

Davido anakuwa msanii wapili nchini Nigeria kumpoteza mtoto kwa kuzama kwenye maji hii ni baada ya kutokea kwa tukio kama hilo kwa msanii D’Banj mnamo mwaka 2018






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags