Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali, Mwalimu huyo huchagua kuogelea kwa kuvuka mto ili kuepuka safari ya kilomita 24 kwa barabara, ambayo inamhitaji kubadilisha mabasi matatu na kuchukua muda mrefu kufika shuleni.
Mwalimu Malik huanza siku yake kwa kuogelea akiwa na mfuko wa plastiki anaobeba nguo zake na vitabu, na baada ya kuvuka mto, hubadilisha nguo na kuendelea na safari ya kuelekea shuleni. Licha ya changamoto hiyo ya kila siku, hajawahi kukosa darasa hata siku moja, akionesha kujitolea kwa hali ya juu katika taaluma yake.

Aidha mpaka mwishoni mwaka mwaka 2023 mwalimu huyo aliendelea kuvuka mto lakini baada ya kupandishwa cheo na kupewa majukumu mapya sasa hutumia barabara kufika shuleni.
Leave a Reply