Usiyoyajua Kuhusu Uendeshwaji Kesi Ya Diddy

Usiyoyajua Kuhusu Uendeshwaji Kesi Ya Diddy

Ikiwa ni wiki mmoja imepita tangu kesi ya rapa wa Marekani, Diddy Combos ikiendelea kuunguruma mahakamani huku baadhi ya watoa mashtaka wakianza kutoa ushahidi akiwemo aliyekuwa mpenzi wa msanii huyo Cassie Ventura.

Kabla ya kesi hiyo kufanyiwa maamuzi na kutolewa hukumu mahakama imetoa wiki sita kwa ajili ya kusikilizwa kwa pande zote mbili, huku mahakama hiyo ikiteua 'Jurors' wengine kufuatilia ushahidi wa kesi hiyo ambapo waamuzi hao walipatikana wiki iliyokwisha.

Jurors 'Waamuzi' ni baraza la watu ambao huchaguliwa kwenda kusikiliza kesi ya mtu, ushahidi na pande zote mshataki na mshatikiwa halafu baadae ndio huja na hitimisho kama mtuhumiwa anahatia au hana.

Baada ya Jurors hao kuchaguliwa hufanyiwa usaili ili kujua kama wanafahamiana kwa vyovyote na muhusika kwenye kesi hiyo au wanaijua historia yake kiundani na pindi Jurors anapoonekana anauhusiano na mtuhumiwa au mshaki huondolewa kwenye baraza hilo lengo ikiwa ni kuondoa upendeleo wowote baina ya pande zote mbili.

Lakini pia, kesi ya Pididy haioneshwi kwenye vyombo vya habari kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya kesi kubwa duniani zinazowahusu watu maarufu huoneshwa kwenye channel ya ‘Law&Crime’ lakini kwa kesi hii haitokuwa hivyo kwa sababu kesi hiyo ni ya shirikisho 'Federal Case'.

Mbali na kesi hiyo kutooneshwa Mubashara (live) lakini ndani ya mahakama wanakuwepo waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu baadhi ili jamii kujua kinacho endelea katika kesi hiyo. Huku wakitumia michoro kuonesha mazingira ya ndani kutokana na kutoruhusiwa kupiga picha.

Kwa mujibu wa waandishi ambao wamehudhuria kesi ya Diddy wanasema rapa huyo anaonekana mwenye kujiamini na anatazama watu machoni bila shaka.

Lakini pia, inaelezwa kuwa mashahidi wengi ambao walitakiwa kutoa ushirikiano katika kesi hiyo hawajatokea mahakamani hapo huku wengine wakizifungia kabisa na kuzitupilia mbali kesi zao.

Kesi hiyo ambayo imeanza kusikilizwa Mei 5, 2025, inatarajiwa kundelea ndani ya wiki sita mfululizo mpaka kupatikane uamuzi wa kuridhisha na endapo itatokea muda huo kesi hiyo haijapata muafaka basi muda utasogezwa mbele.

Utakumbuka Septemba 16,2024 jijini New York , Diddy, alikamatwa na maafisa wa Idara ya Usalama wa Ndani ya Marekani (Homeland Security Investigations). Akishtakiwa kwa makosa matano yakiwemo njama ya kufanya uhalifu (racketeering conspiracy), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, na usafirishaji kwa ajili ya uasherati.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags