Mwanafunzi ajiteka ili apate pesa kutoka kwa wazazi wake

Mwanafunzi ajiteka ili apate pesa kutoka kwa wazazi wake

Kijana mmoja Jijini Nairobi, nchini Kenya anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo kwa kosa la kujiteka ili apate fedha kutoka kwa wazazi wake.

Kijana huyo ajulikanae kama Edwin Kamau (23) ni mwanafunzi wa udaktari, anatuhumiwa kutoweka siku ya Jumapili na kumpigia simu mama yake siku chache baadaye kuomba fidia ya Ksh. 70,000 ambayo ni sawa na Tsh. 1,382,510.

Siku ya Jumatano , kijana alitumiwa awamu ya kwanza ya fedha hizo, lakini Polisi wanasema mwanafunzi huyo alienda kulewa nje kidogo ya Jiji na Mwanamke ambaye aliongeza kinywaji chake na kuiba pesa hizo.


Siku ya Alhamisi, alidai na kulipwa awamu ya pili ya fidia hiyo lakini akamatwa muda mfupi baadaye na pesa hizo zikapatikana zikiwa zimewekwa kwenye viatu vyake, Polisi wanasema mwanafunzi huyo alikiri kufuja pesa zilizokuwa zikilipwa ada ya muhula uliopita na kughushi utekaji nyara wake ili kutafuta pesa.

Kijana huyu yupo rumande akisubiri kufikishwa mahakamani.surprised






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags