Mwanamke mkoani Geita ajifungua katika kituo cha basi

Mwanamke mkoani Geita ajifungua katika kituo cha basi

Mwanamke mmoja mkoani Kigoma ambae ambaye jina hakuweza kufahamika, aliekuwa akitokea Geita mjini akielekea Kasuru amelazimika kukatisha safari yake mara baada ya kupata uchungu ghafla na kujifungua ndani ya Kituo cha Mabasi katika Mji mdogo wa Katoro, Geita.

Mwanamke huyo amesema alianza kuhisi uchungu na kuchukua uamuzi wa kukatisha safari yake ili akatafute huduma ya kujifungua lakini kabla hajaondoka mazingira ya stendi ghafla alijikuta anajifungua Mtoto wa kike katikati ya stendi hiyo.

Baadhi ya Mashuhuda waliokuwepo eneo hilo (Wapiga Debe na Wajasiriamali) wamesema wametoa msaada mkubwa kwa Mama huyo katika kunusuru maisha yake pamoja na kichanga ambapo waliomba moja ya duka la dawa kwa ajili ya kumpa huduma ya kwanza na kumstiri.

Aidha Josephine Skerioni ni Muuguzi katika Kituo cha Afya cha Katoro na amethibitisha uwepo wa tukio hilo na kwamba Mama huyo alifikishwa Kituoni hapo kwa uangalizi zaidi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags