Mzee wa buga kweli ni jipu, angalia matukio alioyafanya mwaka huu

Mzee wa buga kweli ni jipu, angalia matukio alioyafanya mwaka huu

Alooooweeeeh! Alooooohtenaaah! Jamani jamani kumbe kijana wa buga yuko fire kwenye haya matukio kama unavyotujua watu wa bongo yani hatunaga mba mba mba tayari watu washafukua makaburi yote ya mwanamuziki Kizz Daniel ambayo ameshayafanya kupitia show zake za mwaka huu na watu wanasema kuwa ndio tabia yake

Basi bwana matukia ambayo ashayafanya kupitia tour yake hii ya kuzunguka mataifa mbalimbali aliacha gumzo kwa aina yake mpka jana alivyokuwa gumzo nchini Tanzania.

Tukio la kwanza lilikuwa ni Juni 2022: Alizua hasira nchini Zambia, nusura show yake izuiwe kufuatia dharau kwa waandishi wa habari na kumsukuma shabiki yake mmoja aliyejaribu kumpa Maua wakati akiwasili Uwanja wa Ndege.

La pili ni Julai 2022: Alizomewa na Mashabiki Maryland nchini Marekani baada ya kuchelewa kwa masaa manne na kusababisha kutupiwa vitu wakati akitumbuiza jukwaani.

La tatu niJulai 2022: Aliwakasirisha mashabiki wa Denver nchini marekani baada ya kuifuta show yake ambayo aliyakiwa kuifanya ba kupelekea mashabiki kutumia mitandao ya kijamii kumshambulia

Na la mwisho ndo hili la bongo Dar es salaam ambapo ilikuwa ni August 2022: Aliwasilia Tanzania saa chache kabla ya Show huku akishindwa kutumbuiza kwa sababu mbalimbali ikiwemo begi lenye mavazi kusahaulika Airport alikotoka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags