Rick Ross amshukia Drake kuharibika kwa ndege yake

Rick Ross amshukia Drake kuharibika kwa ndege yake

Baada ya ukurasa ujulikanao kwa jina la ‘Keep 6ix Solid” ku-share baadhi ya picha za ndege ya mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross kunusurika na ajali ‘rapa’ Drake ameonekana kufurahishwa na kitendo ambapo amedaiwa ku-like katika posti hiyo.

Kutokana na Drake ku-like katika akaunti hiyo, Rick amerudi tena mitandaoni na kudai kuwa ‘rapa’ huyo huenda akawa sababu ya kuharibika kwa ndege yake hiyo iliyopewa jina la ‘Rick Ross’.

Wawili hao wiki chache zilizopita walikuwa wakitupiana madongo na kutambiana mali wanazozimiliki ambapo Rick alikuwa akieleza kuwa ndege binafsi anayoimiliki Drake kuwa ni ya zamani hivyo inabidi awe makini nayo anapoitumia kwenye safari zake.

Ndege binafsi ya mwanamuziki Rick Ross ilinusurika na ajali jijini Dallas nchini Marekani siku ya jana baada ya kutua vibaya na kuharibika katika baadhi ya sehemu ya ndege hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags