Sopu adondokea AZAM

Sopu adondokea AZAM

Tofauti na watu wengi walivyodhania, mshambuliaji wa Coastal Union, Abdul Suleiman 'Sopu' ameangukia mikononi mwa timu ya Azam FC badala ya Simba au Yanga kama ilivyotegemewa.

Kinara huyo wa mabao Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) alikuwa anawindwa na Simba, Yanga na asubuhi ya leo matajiri hao wa Chamanzi wamemalizana naye.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Azam kimethibitisha usajili wa staa huyo ambaye alikuwa akiitumika Coastal Union, wamelazimika kuvunja mkataba wake wa miaka miwili kwa dau la Sh100 millioni.

"Sopu rasmi ni mali ya Azam, amemalizana nasi muda wowote kuanzia sasa ataweza kutambulishwa huu ni usajili wetu wa tano baada ya kunasa saini za wageni watatu na wazawa wawili," kinasema chanzo hicho.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags