UN: Nchi zilizoendelea zipunguze madeni kwa mataifa masikini

UN: Nchi zilizoendelea zipunguze madeni kwa mataifa masikini

Umoja wa Mataifa (UN) umetoa wito wa kuwepo kwa mabadiliko kutoka nchi zilizoendelea kuyapunguzia mzigo wa madeni yanaoongezeka kwa mataifa masikini zaidi.

Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, Achim Steiner, amesema mgogoro wa madeni unayoyaandama mataifa hayo unatishia maendeleo yaliofikiwa huku yakiyatazama zaidi mataifa ya Afrika na Amerika ya Kusini na kugusia janga la virusi vya korona na mabadiliko ya tabianchi yanayoongeza ukali kwa mataifa hayo.

Katika ripoti ambayo imechapishwa leo, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limebainisha kwamba nchi 54 zinazoendelea zina mzigo mzito wa madeni na zimekuwa zikichangia asilimia 3 tu katika uchumi wa dunia, huku zaidi ya asilimia 50 ya watu wake wakiishi katika umasikini uliotopea.

Nchi zilizoathirika zaidi ni pamoja na Chad, Zambia, Sri Lanka na Pakistan.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags