Urafiki Wa Mke Wa Jux Na Enioluwa Ulianzia Huku

Urafiki Wa Mke Wa Jux Na Enioluwa Ulianzia Huku

Kati ya watu ambao wamepata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania, kutokana na mbwembwe walizofanya kwenye harusi ya msanii Jux na mkewe Priscilla ‘Hadiza’ ni Enioluwa Adeoluwa.

Sherehe hiyo ya harusi ilifanyika Februari 7, 2025 na kuhudhuriwa na watu maarufu mbalimbali kama Diamond Platnumz, Zuchu, Ommy Dimpoz, Billnass na wengineo. Licha ya uwepo wa wote hao, Enioluwa ambaye ni rafiki wa mke wa Jux kutoka Nigeria aliibua mijadala



Urafiki wa Priscilla na Enioluwa ulianzia mwaka 2021 wakiwa katika Chuo Kikuu cha Babcock. Urafiki huo ulishamiri zaidi mwaka 2023, ambapo walikuwa wakionekana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe na kushirikiana katika kazi zao za mitindo.

Baada ya kuwa na urafiki wa karibu zaidi wawili hao walihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi. Hatua hiyo ilimfanya Priscilla kukanusha madai hayo kwenye moja ya mahojiano yake akiweka wazi kuwa Enioluwa ni rafiki yake wa karibu (BFF).

Hata hivyo wawili hao wameonekana katika filamu ya pamoja iitwayo ‘All Of Us’ iliyotoka 2024, ikiwa na mastaa wengine akiwemo mama mzazi wa mke wa Jux, Iyabo Ojo, Kate Henshaw, Jemima Osunde.

Enioluwa Adeoluwa ni nani?

Enioluwa Adeoluwa ‘Lipgloss Boy’ ni mshawishi maarufu wa mitandao ya kijamii, mtayarishaji wa filamu, na mjasiriamali alijulikana zaidi kufuatia mitindo ya mavazi na urembo.



Amekuwa na mafanikio makubwa katika mitandao ya kijamii huku akijipatia maokoto katika kufanya matangazo mbalimbali. Mwaka 2024 umetajwa kuwa ulikuwa wa kutimiza ndoto zake baada ya kuzindua filamu yake ya kwanza ambayo aliitayarisha mwenyewe ‘All Of Us’.

Enioluwa alizaliwa Julai 26, 1999 alihitimu katika Chuo Kikuu cha Babcock kilichopo Ilishan-Remo, Nigeria, ambapo alisomea Masuala ya Vyombo vya Habari na Sanaa ya Maigizo ('Media and Theater Arts') na kuhitimu 2021.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags