Usher ataka kuwa sehemu ya Afrobeat

Usher ataka kuwa sehemu ya Afrobeat

Mkali wa R&B kutoka nchini Marekani, Usher ameweka wazi kuwa anataka kuwa sehemu ya muziki wa Afrobeat. 

Hii inakuja baada ya kuvutiwa na uimbaji wa wasanii kutoka nchini Nigeria, ambapo tayari ameshafanya ‘kolabo’ na mwanamuziki Burna Boy na Pheelz katika album yake mpya ya ‘Home Coming’.

Kupitia mahojiano yake na Apple Music, Usher ameeleza kuwa anampango wa kufanya ‘kolabo’ zaidi na wasanii wa Nigeria na kupeleka utamaduni wa Africa Marekani kutokana ngoma zao kuwa maarufu duniani kote hivyo basi amedai kuwa anataka kuwa sehemu ya muziki wa Afrobeat.

Ukiachilia mbali wasanii wa Nigeria, mkali huyo wa R&B kwa hapa Tanzania ameomba kufanya ‘kolabo’ na mwanamuziki Nandy kupitia wimbo wa ‘Dah’, ambapo mpaka sasa bado haijafahamika rasmi remix hiyo itaachiwa lini.  

Muziki wa Afrobeat au kwa jina lingine ‘Afrofunk’ ni aina ya muziki wa Kinaigeria ambao unahusisha mchanganyiko wa mitindo ya muziki wa kitamaduni wa Kiyoruba na Igbo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post