Mwanamuziki wa Nigeria Tems ameibuka mshindi wa Grammy 2025 katika kipengele cha Best African Music Perfomance.
Ushindi huo ambao ameupata usiku wa kuamkia leo Februari 3, 2025 kupitia wimbo wa Love Me Jeje, unaenda kuwa wa pili baada ya mwaka jana kushinda katika kipengele cha Best Melodic Rap Perfomance ‘Wait For You’.
Hata hivyo ushindi wa Tems unaenda kuzalisha deni kwa Davido kwani jana Februari 2,2024 aliahidi kuwa endapo asipoondoka na Grammy 2025 ataacha kufanya muziki.
"Kama sitoshinda Grammy mwaka huu ninafikiria kuacha muziki, nimeweka moyo wangu na roho yangu kwenye kazi, najituma kuliko msanii yeyote ndani ya Africa. Daima mimi ndiye huwa mbele naiongoza Afrobeat, naongoza mashambulizi, naitengeneza aina hii ya muziki.
“Mimi ndiyo jina kubwa kwenye Afrobeat, hilo halina mashaka, lakini kabati langu la tunzo haliakisi machozi, jasho na damu nilivyowekeza. Kuchaguliwa kugombea Grammy kwa miaka 2 mfululizo kumenipa furaha, lakini pia hii ni dawa chungu kuimeza. Kama Grammy wangekua kweli wanausawa, ningeshachukua takribani tunzo 20 hadi hivi sasa,"amesema Davido
Utakumbuka Davido aliwania kipengele cha Best African Music Performance ambacho ameshinda Tems
Wasanii wengine waliochuwana na Tems ni Burnaboi 'Higher', Chris Brown & Lojay 'Sensational', Yemialade 'Tomorrow', pamoja na Asake & Wizkid MMS
Leave a Reply