Utajiri wa Jackie Chan hauwahusu Watoto wake

Utajiri wa Jackie Chan hauwahusu Watoto wake

Mwigizaji wa Hong Kong Jackie Chan ametangaza nia ya kuchangia utajiri wake wote, unaokadiriwa kufikia dola 400 milioni 'Sh 966 bilioni', kama msaada kwa watu wenye uhitaji.

Mwigizaji huyo ameshangaza wengi akizungumza na jarida la Wealth baada ya kutangaza kuweka mirathi yake kama hisani kwa ajili ya kusaidia watu hao huku akiwataka watoto wake kujitengenezea pesa zao wenyewe.

"Akijua uwezo wake anaweza kutengeneza pesa zake mwenyewe. Asipokuwa na uwezo basi atakuwa anapoteza pesa zangu tu," alisema Chan.

Hata hivyo mwigizaji huyo ameelezea alivyopitia wakati mgumu kipindi cha ukuaji wake. Hivyo furaha yake ni kusaidia wengine.

"Nikimpatia mtu furani kitu na nikamtamzama usoni huwa najisikia furaha," amesema Chan

Ikumbukwe katika kipindi chote cha mafanikio ya kazi zake, Chan amekuwa akishiriki kikamilifu katika shughuli za kutoa misaada kwa watu na makundi yenye uhitaji. Hiyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha taasisi yake binafsi ya 'Jackie Chan Charitable Foundation' mwaka 1988.

Taasisi hiyo ipo kwa lengo la kusaidia watu katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanikisha elimu na majanga kama mafuriko, ajali n.k.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags