Shirika la Afya duniani (WHO) limetaja nchi ambazo zimeathirika na ugonjwa wa kipindupindu, ambapo shirika hilo limesema kuwa ugonjwa huo umeenea duniani kote, haswa barani Afrika na hali imekuwa mbaya zaidi tangu tathmini yake ya mwisho ya mwezi Februari.
Nchi nne zinaripoti kuwa na kesi za ugonjwa huo ambazo ni Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini na kufanya kufikia jumla ya nchi 24 zinazosumbuliwa na tatizo hilo.
Sehemu ambazo milipuko imeenea zaidi inabaki kuwa Malawi, Msumbiji, na Somalia.
Shirika hilo limeeleza kuwa upungufu wa chanjo ya kipindupindu ya kunywa na huduma za afya kuwa na uwezo mdogo wa kukabiliana na hali inayozidi kuwa mbaya.
Leave a Reply