Zaidi ya wanafunzi 1000 wa sekondari waacha shule kwa mwaka 2022

Zaidi ya wanafunzi 1000 wa sekondari waacha shule kwa mwaka 2022

Wanafunzi 1,648 wa shule za sekondari wameacha shule kwa mwaka 2022 mkoani Mtwara huku waliotokea vijijini wakiwa wengi zaidi.

Wanafunzi hao wa kidato cha pili na cha nne, Wilayani Newala, wameacha shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba, kuhama kwa wazazi kwa ajili ya kilimo, hali ngumu ya maisha, wazazi kutengana na wenyewe kutokuwa na mwamko wa elimu.

Aidha Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira wa Wilaya hiyo, Mwl. Bashiru Malocho ameeleza wanafunzi 881 ni kutoka kidato cha pili na wanafunzi 767 ni kidato cha nne, huku 1,031 wakitokea Newala Vijijini na 617 Newala Mjini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags