Zerobrainer Ashinda Tuzo South Afrika

Zerobrainer Ashinda Tuzo South Afrika

Mtanzania anayefanya maudhui ya vichekesho kupitia mpira wa miguu Zerobrainer ashinda tuzo ya Sports Creator of the Year TikTok Awards 2024 zilizofanyika Johannesburg South Afrika.

Zero amewashukuru timu yake anayofanya nayo kazi, mashabiki wake waliofanikisha kushinda kwa kumpigia kura kwenye tuzo hizo.

"Ni upendo na sapoti kutoka kwenu mashabiki wangu wapendwa hatimaye kufika hapa. Ninashukuru timu yangu kwa bidii na ubunifu wa maudhui ambayo yalitufanya tupigiwe kura kama Muundaji Bora wa Michezo wa Mwaka kwenye TikTok 2024" amesema Zero.

Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amempongeza kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo.

“Kongole Zerobrainer0 kwa kushinda tuzo ya Sports Creator of the Year 2024 ukiwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hii. Ubunifu, juhudi na maarifa vinalipa. Heshima kwako na heshima kwa Tanzania. Wafuasi wako tumefurahi,”ameandika Msigwa katika ukurasa wake wa Instagram.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Mtanzania kushinda tuzo hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags